Kwa kawaida, watu husema kwamba mtu mkuu ni yule mwenye mali, heshima na mamlaka. Lakini Mungu ana mtazamo tofauti kabisa. Ni mtu wa aina gani anayeweza kuitwa mkuu machoni pa Mungu?
Kwanza, mtu mkuu hujinyenyekeza na kuwatumikia wengine. Yesu alisema katika Mathayo 18:4, “Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni,” na katika Mathayo 20:26–27, “Mtu ye yote anayetaka kuwa mkuu kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu.” Watu husema tunaweza kupandishwa tunapojipandisha wenyewe, lakini tukijishusha na kutenda kwa unyenyekevu tutadharauliwa.
Hata hivyo, kweli inatufundisha kwamba mtu anayejishusha na kuwatumikia wengine anaweza kutambuliwa na Mungu kuwa mkuu. Nyakati nyingine huonekana kwamba mtu anayejitukuza na kutaka kuhudumiwa ndiye mkuu, lakini mtu mnyenyekevu wa kweli anayewatumikia wengine hatatambuliwa duniani tu; Mungu pia atamtukuza.
Pili, mkuu ni yule anayefundisha na kutenda Neno la Mungu. Yesu alisema katika Mathayo 5:19, “Basi mtu ye yote atakayevunja amri mojawapo katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.” Ukiona neno lolote la Mungu kuwa dogo na lisilo na umuhimu na kuwafundisha wengine kwamba hawahitaji kulitii, utaitwa mdogo kabisa mbinguni.
Unapaswa kuthamini kila neno la Biblia na kuwafundisha wengine kulitenda na kuishi kulingana nalo. Hata kama unaweza kulifundisha Neno la Mungu vizuri kiasi gani, huwezi kuitwa mkuu usipotenda kulingana nalo. Utaitwa mkuu mbinguni tu unapowafundisha wengine Neno la Mungu huku ukilitenda mwenyewe.
Tatu, mkuu ni yule anayetembea pamoja na Bwana wetu katika majaribu. Yesu alipokuja duniani na kupitia majaribu, wanafunzi wake walimfuata na kuwa pamoja naye katika majaribu yake. Alipokuwa na njaa, wao pia walikuwa na njaa; na alipoonewa na watu waovu, wao pia waliteswa kwa ajili ya jina lake. Yesu aliwaahidi katika Luka 22:28–30, “Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. Nami nawawekea ninyi ufalme, kama Baba yangu alivyoniwekea mimi, mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.” Ahadi hii inamhusu kila anayeteswa kwa ajili ya haki katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo kwa sababu analishika Neno la Mungu.
Mateso hayo hutokea, kwa mfano, mtu anapoacha anasa za dunia alizofurahia na marafiki wa kidunia na kuanza kuishi maisha ya kumcha Mungu; au anapoanza kuhudhuria ibada mbalimbali na mikutano ya maombi pamoja na ibada ya Jumapili, ilhali hapo awali hakuiheshimu Siku ya Bwana. Kama 1 Yohana 4:18 inavyosema, “Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu.” Ukiwa na upendo kamili kwa Mungu, hofu hutoweka na unaweza kushiriki katika majaribu ya Bwana.
Ninaomba kila mmoja wenu awafundishe wengine Neno la Mungu kwa unyenyekevu na kulitii, na pia ampende Mungu kikamilifu ili aitwe mkuu mbinguni. Ninaomba haya katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo!
His Emeritus Bishop Dr. Jaerock Lee
Yule mwana mdogo akakusanya vitu vyake vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali, na huko akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa. Mmoja wao, mwana mdogo, akamwambia baba yake, “Baba,
Mfalme na maafisa wake walimwacha Mungu na kuabudu sanamu. Ghadhabu ya Mungu ikawajia watu wa Yuda, nao wakavamiwa na jeshi la Waaramu.
Upendo hautafuti faida yake mwenyewe, bali hujitoa kwa ajili ya wengine. Huo ndio upendo wa kweli wa kiroho usiobadilika milele. Mungu anataka tuishi katika wema na haki, na kuitimiza Sheria kwa upendo.